Dini ya Kiislamu kuipiku ile ya Kikristo kwa ukubwa 2070


Waislamu wakifanya ibada. Utafiti unasema kuwa dini ya Uislamu inatarajiwa kuipiku ile ya Wakristo ifikiapo 2070

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Waislamu wakifanya ibada. Utafiti unasema kuwa dini ya Uislamu inatarajiwa kuipiku ile ya Wakristo ifikiapo 2070

Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa baada ya Ukristo kwa sasa lakini inakua kwa haraka sana.

Hata hivyo hilo huenda likabadilika iwapo mwenendo wa watu wanaojiunga na dini hiyo utaendelea, kulingana na utafiti uliochapishwa na kituo cha utafiti cha Marekani Pew Research Center.

Kulingana na utafiti huo Uislamu unakuwa kwa haraka ikilinganishwa na dini nyengine yoyote ile duniani.

Itaipiku dini ya Kikristo ifikiapo 2070 kulingana na makadirio yake na hivyobasi kuwa dini yenye ufuasi mkubwa duniani.

Mwaka 2010 taifa la Indonesia ndilo taifa lililokuwa na idadi kubwa ya Waislamu duniani lakini sasa India huenda ikawa na wafuasi wengi zaidi duniani ifikiapo 2050.

Hatahivyo taifa hilo litakuwa na wafuasi wengi wa dini ya Hindu.

Papa Francis ,kiongozi wa kanisa katoliki duniani

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Papa Francis ,kiongozi wa kanisa katoliki duniani

Idadi ya Wakristo nchini Uingereza na Ufaransa itashuka kwa asilimia 50 na asilimia 10 ya watu wanaoishi Ulaya wanakadiriwa kuwa Waislamu kufikia 2050.

Wanne kati ya Wakristo 10 duniani watakuwa wakiishi katika jangwa la sahara barani Afrika.

Na nchini Marekani mmoja kati ya watu 50 watakuwa Waislamu kufikia 2050.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?