Robert Kelly: Nyota wa muziki wa R&B nchini Marekani maarufu R. Kelly apatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono


Kelly hapa anaonekana akiingia mahakamani Juni 2019

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Maelezo ya picha, 

Kelly hapa anaonekana akiingia mahakamani Juni 2019

Mwimbaji wa Marekani R Kelly amepatikana na hatia ya kutumia hadhi yake ya kuwa nyota wa muziki wa R&B kuendesha mpango wa kuwadhulumu kingono wanawake na watoto kwa zaidi ya miongo miwili.

Walalamishi 11, ikiwemo wanawake tisa na wanaume wawili, walitumia wiki sita kuelezea udhalilishaji wa kingono na ghasia walizokumbana nazo mikononi mwake.

Baada ya siku mbili ya majadiliano, jaji alimpata R Kelly na hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa anakabiliwa nayo.

Hukumu dhidi yake itatolewa Mei 4 na huenda akafungwa maisha.

Majaji walimpata Kelly, ambaye jina lake kamili ni Robert Sylvester Kelly, kuwa kiongozi wa mpango hatari uliyowavutia wanawake na watoto na hatimaye kuwanyanyasa kingono.

Mwimbaji huyo - maaarufu wa wimbo wa I Believe I Can Fly ulioshinda tuzo - pia aligundulika kuwasafirisha wanawake kati ya majimbo tofauti ya Marekani na kuandaa filamu ya ponografia ya watoto.

Mwanamke mmoja aliyetoa ushahidi kuwa Kelly alimfunga, kumpatia dawa za kulevya na kumbaka alisema katika taarifa iliyoandikwa baada ya uamuzi huo kwamba amekuwa "akijificha" "kutokana na vitisho vilivyotolewa dhidi yangu" tangu alipomtuhumu hadharani.

"Niko tayari kuanza maisha huru bila uwoga na kuanza mchakato wa uponyaji," mwanamke aliyetambuliwa mahakamani kama, Sonja, aliongeza.

Nyaraka za kisheria pia zilifichua mateso ya kiakili ambayo Kelly aliwafanyia wahasiriwa wake. Hawakuruhusiwa kula au kwenda msalani bila idhini yake, aliamua nguo walizovaaa na kuwafanya wamuite "Daddy".

Gloria Allred, wakili aliyewawakilisha wahasiriwa kadhaa, aliwaambia waandishi: "Nimehudumu kwa miaka 47. Wakati huu, nimefuatilia wanyanyasaji wengi wa kingono ambao wamefanya uhalifu dhidi ya wanawake na watoto 

"Kati ya wanyanyasaji wote niliowafuatilia , Bw. Kelly ni mbaya zaidi."

Maelezo ya video, 

Tazama: R. Kelly \"ni mnyanyasaji hatari zadi wa kingono.\"

Katika mkutano na wanahabari nje ya mahakama siku ya Jumatatu, mwendesha mashtaka Jacquelyn Kasulis alisema kuwa jaji alituma ujumbe mkali kwa wanaume wengine wenye uwezo kama Kelly.

"Haijalishi itachukua muda gani, mkono mrefu wa sheria utakunasa,"alisema Bi. Kasulis.

Uamuzi huo unakuja miaka 13 baada ya Kelly kufutiwa mashtaka ya ponografia ya watoto baada ya kushtakiwa katika jimbo la Illinois.

Madai mengi yaliyosikilizwa katika kesi hiyo yalitolewa kwanza katika simulizi ya mwaka 2019 ya Surviving R Kelly.

Wahasiriwa wakati mwingine waliteuliwa miongoni wa watu waliohudhuria tamasha lake, au walishawishika kuungana naye baada ya kupewa msaada na kazi zao mpya za muziki baada ya kupata bahati ya kukutana na mwimbaji huyo.

Lakini baada ya kujiunga na wasaidizi wake, waligundua kwamba walikuwa chini ya sheria kali na waliadhibiwa vikali ikiwa walikiuka kile timu yake iliita "Sheria za Rob".

2px presentational grey line

2px presentational grey line

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?