Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kombe la dunia : Afrika haina viwanja vya mechi za kombe la dunia


africa

CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES

Kupigwa marufuku kwa viwanja kadhaa vya soka barani Afrika huenda kutaathiri mechi za ufunguzi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la Afrika mnamo Juni.

Jumla ya mataifa 10 kati ya 40 yanayoshiriki katika kampeni ya kufuzu yanakabiliwa na tishio la kushiriki mechi nje ya mipaka yao .

Hii ni baada ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kutuma barua kwa mashirikisho wanachama wiki hii iliyokuwa na orodha ya viwanja vilivyoidhinishwa kwa raundi mbili za kwanza za mechi za makundi.

Nchi zilizoathiriwa ni pamoja na Senegal, ambao walishiriki kwenye Kombe la Dunia lililopita huko Urusi mnamo 2018, na Mali, ambao walikuwa miongoni mwa timu zilizoshinda nafasi ya kwanza.

Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Liberia, Malawi, Mali, Namibia, Niger na Sierra Leone zote hazijaidhinishiwa viwanja vyao vya nyumbani wakati Caf inapokabiliana na miundombinu mibovu kote barani.

Sasa timu hizo zina muda mfupi sana kabla ya tarehe ya mwisho kuboresha viwanja vyao kabla ya mechi ya kwanza mnamo 5 Juni au watalazimika kuchezea mahali pengine.

Senegal inafungua kampeni yao ya Kundi H nyumbani dhidi ya Togo wiki ya kwanza ya Juni, lakini Uwanja wao maarufu wa Leopold Senghor umefungwa kwa ukarabati na kumbi mbadala zinazotumiwa kwa wachezaji wa kimataifa waliotangazwa kutostahili na kulingana na CAF

DR Congo, Libya na Uganda wamekataliwa viwanja vyao lakini bado wataweza kucheza nyumbani kwenye viwanja vidogo, mbadala.

Awamu ya makundi ya utangulizi wa Kombe la Dunia la Afrika ina nchi 40 zilizogawanywa katika vikundi 10 vya timu nne. Watacheza mechi sita kila hadi Oktoba.

Mwezi Novemba, washindi wa makundi wataungana kwa mechi tano za mchujo na washindi wa jumla watafuzu kwa fainali zitakazofanyika Qatar mwakani.

Soka barani Afrika limeathiriwa kwa muda mrefu na vifaa duni vya uwanja na viwanja vya kiwango cha chini na Caf imeonesha uthabiti zaidi katika kupiga marufuku viwanja visivyo na ubora unaohitajika .

Lakini mnamo Machi, marufuku kama hiyo kwa viwanja kadhaa barani kote kwa raundi ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika iliondolewa dakika ya mwisho. Caf haikutoa ufafanuzi kuhusu kubadilisha uamuzi wake 

Marufuku ya Fifa dhidi ya Zoo Kericho 

zoo kericho

CHANZO CHA PICHA, FACEBOOK-ZOO FC

Kwingineko klabu ya ligi ya premia nchini Kenya Zoo Kericho itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Fifa wa kuwafukuza kutoka Ligi ya Shirikisho la Soka Kenya katika msimu wa mwaka wa 2020/21.

Shirikisho la soka ulimwenguni fifa liliamuru klabu hiyo yenye makao yake Kericho kuondolewa katika ngazi ya juu baada ya kupatikana na hatia ya "utapeli wa mechi".

Fifa pia iliamuru FKF kushusha Zoo mara moja kwa Ligi ya Daraja la Kwanza ya FKF kwa msimu ujao. Hizo ni darafa mbili chini ya safu kuu ya soka nchini Kenya .

"Kamati ya Nidhamu ya Fifa inaona kilabu cha Zoo FC kuwajibika kwa shughuli zinazohusiana na utapeli wa mechi na mashindano " Fifa ilisema kupitia barua .

Lakini mmiliki wa Zoo Ken Okoth anasema watatumia kikamilifu dirisha la siku 30 la kukata rufaa kuwasilisha malalamiko katika Korti ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) chini ya hati ya haraka 

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?