Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2021

Panya wa Tanzania wagundua kifua kikuu

Picha
Kifua Kikuu ni moja wapo ya magonjwa sugu duniani ya kuambukiza. Ugonjwa huu wa TB husababisha vifu vya zaidi ya watu milioni 1.5 kila mwaka huku wengine bilioni 1.7 wakiambukizwa.  Shirika la Afya Duniani(WHO) linasema nchi masikini nyingi kutoka Afrika ndizo zilizoathirika na maambukizi ya TB. Nchini Tanzania utafiti maalum umeanzishwa ambapo wanasayansi wanatumia Panya kuchunguza TB na kuanza mapema matibabu yake.  Waandishi  Dayo Yusuf na Munira Hussein walitembelea kwenye maabara moja kunakofanyiwa utafiti huu mjini Dar es Salaam na kuandaa taarifa ifuatayo. Follow us on Facebook Follow us on Instagram Follow us on Twitter

Hatua gani zichukulie dhidi ya wachezaji kushambiliana(kupigana) wakati wa mchezo?

Picha
TAZAMA: Kipa wa timu ya Glentoran Aaron McCarey akimshambulia mlinzi wake baada ya kushindwa kuzuia bao Kipa wa klabu ya Glentoran Aaron McCarey aonekana akimkaribia na kumshambulia mchezaji wa timu yake kwa kushindwa kuzuia goli, Tunauliza je inapofikia hatua hiyo ni kipi kinachofanyika? Follow us on Facebook Follow us on Instagram Follow us on Twitter

Tetesi za soka Barani Ulaya:

Picha
Michezo Imepakiwa mnamo 11:37 PSG v Man City: Je Messi kumaliza zimwi la ukame wa magoli dhidi ya kikosi cha Pep Guardiola leo? Ulikuwa ni uhusiano wenye mafanikio makubwa zaidi wa kocha na mchezaji wake katika nyakati za soka la sasa. Tetesi za soka Ulaya Jumanne 28.09.2021: Phillips, Rice, Porro, Kessie, Isco, Jovic, Davies, De Ligt CHANZO CHA PICHA,  JUSTIN TALLIS/GETTY IMAGES Manchester United imeamua kuelekeza nguvu zake kwa kiungo wa Leeds United Kalvin Phillips, 25, baada ya kuachana na mipango yao ya kumsajili kiungo mwenzake wa England Declan Rice, 22, kutoka West Ham. (Star) West Ham ina mpango wa kumuuza Rice kwa dau la £90m ikijiandaa na dau la kumpata mrithi wake. (Football Insider) Real Madrid wanafikiria kupeleka ofa kwa ajili ya mlinzi wa pembeni wa Hispania Pedro Porro, 22, ambaye yuko kwa mkopo Sporting Lisbon akitokea klabu ya Manchester City. (O Jogo - in Portuguese) Follow us on Facebook Follow us on Instagram Follow us on Twitter

Robert Kelly: Nyota wa muziki wa R&B nchini Marekani maarufu R. Kelly apatikana na hatia ya unyanyasaji wa kingono

Picha
CHANZO CHA PICHA,  GETTY IMAGES Maelezo ya picha,  Kelly hapa anaonekana akiingia mahakamani Juni 2019 Mwimbaji wa Marekani R Kelly amepatikana na hatia ya kutumia hadhi yake ya kuwa nyota wa muziki wa R&B kuendesha mpango wa kuwadhulumu kingono wanawake na watoto kwa zaidi ya miongo miwili. Walalamishi 11, ikiwemo wanawake tisa na wanaume wawili, walitumia wiki sita kuelezea udhalilishaji wa kingono na ghasia walizokumbana nazo mikononi mwake. Baada ya siku mbili ya majadiliano, jaji alimpata R Kelly na hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa anakabiliwa nayo. Hukumu dhidi yake itatolewa Mei 4 na huenda akafungwa maisha. Majaji walimpata Kelly, ambaye jina lake kamili ni Robert Sylvester Kelly, kuwa kiongozi wa mpango hatari uliyowavutia wanawake na watoto na hatimaye kuwanyanyasa kingono. Mwimbaji huyo - maaarufu wa wimbo wa I Believe I Can Fly ulioshinda tuzo - pia aligundulika kuwasafirisha wanawake kati ya majimbo tofauti ya Marekani na kuandaa filamu ya ponografia ya watoto. Mw

Anaconda: Nyoka hatari asiyeua kwa sumu

Picha
Katika spishi ya nyoka hatari Zaidi duniani hakuna anayetisha Zaidi kama nyoka wa Anaconda ambaye hufahamika kama Green anaconda au Giant anaconda . Filamu nyingi zimetolewa kuelezea hatari ya nyoka huyu lakini sifa za hatari yake ni Zaidi ya ukubwa wake ambao huwatisha wengi. Nyoka huyu hupatikana Marekani Kusini na cha kushangaza haui kwa sumu bali ana nguvu na misuli ya kipekee kumbana adui wake hadi kufa na kisha kumla mzima . Viumbe sita wenye uwezo wa kuishi kwa maelfu ya miaka kabla ya kufa Unawajua viumbe 10 wa ajabu na wa kutisha wanaoishi baharini? Wanyama watano ambao hufa baada ya kujamiiana Je unayajua yapi kuhusu anaconda? Kulingana na simulizi ya Makala maalum kumhusu nyoka huyo iliyochapishwa na BBC Earth ,anaconda anaweza kuwa na urefu wa hadi futi 25 na uzito wa hadi kilo 136 . Nyoka huyu ndiye mzito zaidi wa aina yake na wakati mwingi anaishi maji au karibu na maji ambako anafanya mawindo yake . Chakula na makazi Nyoka wa anaconda hupenda kuishi karibu na maji na wan

Afghanistan: Fahamu makampuni makubwa ya Marekani yaliojitajirisha na vita vya taifa hilo

Picha
CHANZO CHA PICHA,  GETTY IMAGES Maelezo ya picha,  Kwa kila mwanajeshi mmoja wa Marekani kulikuwa na wanakandarasi wawili Ilikuwa vita ya muda mrefu zaidi katika historia ya Marekani, lakini moja kati ya vita zilizogharimu mapesa mengi.  Vita vya Afghanistan, vilivyohitimishwa Agosti 30 mwaka huu baada ya vikosi vya Marekani kuondoka Kabul, imeigharimu Marekani dola bilioni $ 2.3 billion, kwa mujibu wa Chuo kikuu cha Brown huko kisiwani Rhode. Kurejea madarakani kwa kundi la Taliban nchini Afghanistan na kuondoka kwa vikosi vya Marekani nchini humo kunaonekana na wachambuzi wengi kama ishara ya kwamba ni vita ambayo haikuwa na mafanikio. Kwa wengi inaonekana kama vita isiyo na mafanikio, lakini kwa wengine ilikuwa fursa ya kutengeneza faida kubwa. Fahamu jinsi Taliban walivyoyashinda mataifa yenye uwezo mkubwa duniani Wafahamu mawaziri wapya wa serikali mpya ya Taliban nchini Afghanistan Mfahamu \"Taliban wa Marekani\" aliyekutana na Bin Laden kabla ya 9/11 Kati ya dola trili