Ukigundua una dalili hizi 10 nenda ukapimwe maradhi ya Kisukari
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Afroza Akhtar hakuelewa kwamba alikuwa na kisukari kwa muda mrefu. Hakujua kwamba sababu za kujihisi kiu, uchovu na mwili kuishiwa nguvu huenda ni baadhi ya dalili za maradhi hayo. ''Nilikwenda kwa daktari na kumueleza baada ya kujisikia vibaya kwa muda mrefu.Alinifanyia vipimo vya kisukari na magonjwa mengine. Ni pale ndipo niligundulika kuwa nina ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu '' Tangu hapo alianza matibabu katika hospitali maalum ya ugonjwa wa kisukari. Si yeye pekee, kwa mujibu wa wataalamu wa kisukari, zaidi ya asilimia 50 ya watu wenye maradhi ya kisukari hawafahamu kuwa wana ugonjwa huo MATANGAZO Ugonjwa huo uligunduliwa wakati wa alipokuwa akipimwa maradhi mengine. Unaweza pia kusoma Ni rahisi kuepuka ugonjwa wa kisukari? 14 Novemba 2021 Ugonjwa wa kisukari unaweza kutibika na kuzuiwa kirahisi - Daktari anaeleza 7 Machi 2024 Wataalamu wanasema kutokana na hali hiyo ndiyo maana ni muhimu sana kutoa hamasa kwa jamii kuhusu ugonjw...