Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2024

Hezbollah yasema italipiza kisasi dhidi ya Israel baada ya shambulio la vifaa vya mawasiliano

Picha
BBC News,  Swahili Ruka hadi maelezo Yaliyomo Habari Michezo Makala Afya Burudani Video Vipindi vya Redio MATANGAZO CHANZO CHA PICHA, EPA Saa 4 zilizopita Kundi la Hezbollah la Lebanon limesema katika taarifa yake siku ya Jumatano kwamba Katibu Mkuu wa kundi hilo, Hassan Nasrallah, atatoa hotuba siku ya Alhamisi, kufuatia milipuko ya vifaa vya mawasiliano kote Lebanon siku ya Jumanne. Hezbollah imeahidi "kuendeleza operesheni zake za kijeshi dhidi ya Israel kwa kuunga mkono Ukanda wa Gaza" siku moja baada ya milipuko ya vifaa vya mawasiliano vya wanachama wake. Chama hicho kilisema katika taarifa yake kwamba uungaji mkono kwa Gaza ni tofauti na kile ulichokitaja kuwa ni adhabu kali ijayo kwa adui mhalifu kwa mauaji ya siku ya Jumanne. Hezbollah inaomboleza vifo vya wapiganaji wake wanane, akiwemo mtoto wa Mbunge wa Hezbollah, Ali Ammar. Waziri wa Afya wa Lebanon, Firas Al-Abyad alisema idadi ya watu waliojeruhiwa kutokana na milipuko hii ni watu 2,750, pamoja na waliokufa tis

Urusi yakaribia kudhibiti mji muhimu wa Ukraine

Picha
            Oparesheni ya Kyiv kwenye mji wa Kursk yadhoofika CHANZO CHA PICHA, REUTERS Dakika 38 zilizopita Urusi imepiga hatua kubwa katika siku za hivi karibuni ambayo inatishia kuzidi mafanikio yaliyopatikana na Ukraine katika shambulio lake la mpakani kwenye eneo la Kursk. Vikosi vya Urusi viko kilomita chache tu kutoka mji wa Pokrovsk wa Ukraine, ambao ni muhimu sana kwaajili ya usafirishaji unaotumiwa na jeshi la Ukraine. Pokrovsk ni mji wenye kituo muhimu cha usafiri wa reli na barabara kuu, na ni sehemu muhimu ya usambazaji na uimarishaji kwa wanajeshi wa Ukraine waliopo mstari wa mbele kwa upande wa Mashariki. Wakosoaji ndani ya Kyiv wanahofia kuwa jeshi la nchi hiyo limefanya makosa makubwa. MATANGAZO Hatua ya kutuma wanajeshi kuvamia Kursk badala ya kuimarisha mstari wa mbele wa upande wa Mashariki, kumeacha Pokrovsk na miji mingine muhimu ya Ukraine kuwa hatarini, wakosoaji wanasema. Rais wa Urusi Vladimir Putin alianza rasmi uvamizi wa Ukraine mnamo Februari 2022. Akiwa k