Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Je, Iran ina nguvu ya kuingia vitani moja kwa moja na Israel?


Je, Iran ina nguvu ya kuingia vitani moja kwa moja na Israel?
i

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Suali linaloulizwa na wengi, ni ikiwa Iran inao uwezo wa kuingia vitani na Israel

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameionya hadharani Israel - ni lazima isitishe mashambulizi yake huko Gaza la sivyo italazimika kuchukua hatua.

Ndani ya masaa machache baadaye, Iran ilibadilisha msimamo katika Umoja wa Mataifa - ikasema haitaingilia mzozo kati ya Israel na Hamas ila ikiwa tu maslahi ya Iran na raia wake yataathirika.

Hata hivyo, katika mzozo huu wa pande mbili, Iran tangu awali imeeleza wazi uungaji mkono kwa kundi la wapiganaji wa Hamas na Wapalestina. Pia inaionya Israel huenda ikakabiliwa na matokeo mabaya.

Naibu kamanda wa jeshi la Iran, aliitishia Israel kwa shambulio la kombora katika mji wa Haifa nchini Israel.

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema iwapo mashambulio ya Israel dhidi ya Gaza yataendelea hakuna mtu atakayeweza kuwazuia Waislamu, kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na shirika la habari la Iran Press TV.

Swali la sasa ni iwapo Iran, ambayo mara kwa mara inatoa vitisho na maonyo kwa Israel, kweli ina uwezo wa kupigana na Israel.

Iran, Hamas na Israel

JJ

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Israel inasisitiza Iran haipaswi kuwa na silaha za nyuklia

Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ya mwaka 1979 yalileta madarakani uongozi uliozipa changamoto nchi za Magharibi. Tangu wakati huo, viongozi wa Iran huzungumzia kuangamizwa kwa Israel.

Vile vile Iran haijatambua taifa la Israel. Iran pia inaisema Israel kwa kuendelea kukalia kwa mabavu ardhi za Waislamu.

Israel kwa upande wake inaiona Iran kama tishio. Inasisitiza Iran inataka kutengeneza silaha za nyuklia.

Ingawa Iran na Israel hazijapakana, lakini mvutano kati ya mataifa hayo mawili unaendelea. Iran ina uungwaji mkono wa Lebanon, Syria, na Palestina zinazopakana na Israel.

Baada ya Hamas kuishambulia Israel. Israel iliishutumu Iran kwa kutumia ushawishi wake kuanzisha mashambulizi dhidi ya Israel.

Vyombo vya habari vya nchi za Magharibi viliripoti kuwa Hamas iliiarifu Iran kabla ya shambulio hilo dhidi ya Israel. Na Waziri wa mambo ya nje wa Iran aliztembelea Iraq, Lebanon na Qatar na kukutana na maafisa wa ngazi ya juu wa Hamas baada ya shambulizi kuanza.

Ingawa Iran haiko nyuma ya shambulio hilo moja kwa moja. Wataalamu wanaamini imetoa msaada, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo na kuwapa silaha Hamas.

Iran inaweza kupigana na Israel?

J

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Rais wa Iran Ibrahim Raisi

Mtaalamu wa Masuala ya Asia Magharibi katika Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, Delhi, Profesa Ashwini Mahabatra, anasema:

"Iran imeendelea katika uwanja wa teknolojia kuliko hapo awali. Wana droni na makombora ya masafa marefu. Ingawa Israel inaweza kukabiliana nayo, ila inapendelea kuepuka mzozo na Iran.''

Israeli pia wana silaha. Vilevile inaungwa mkono na Marekani. Popote vita vitapiganwa, Marekani itatoa msaada wake kwa Israel. Katika kesi hii, sidhani kama Iran inataka vita vya moja kwa moja na Israel," anasema.

Profesa Pramanand Mirasra, wa chuo kikuu cha kiislamu cha Jamia Millia anatoa hoja sawa na hiyo: "Iran hakika haitahusika katika vita vya moja kwa moja kwa sababu Israel inaungwa mkono na Marekani. Kwa hivyo, haina uwezo wa kupigana na nchi mbili kwa wakati mmoja."

Kando na hayo, mazingira ya kisiasa ya ndani ya Iran yanaweza yasiiruhusu nchi hiyo kuingia vitani moja kwa moja.

Hamas na Hezbollah ni tishio zaidi kwa Israel?

O

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Iran inaunga mkono makundi ya wanamgambo yanayopigana na Israel

Iran na Israel zimekuwa kwenye mvutano kwa muda mrefu. Nchi zote mbili hadi sasa zimeepuka vita vya moja kwa moja, ingawa nchi zote mbili zimeanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Iran inaendelea kuunga mkono makundi yenye silaha yanayolenga Israel - inaunga mkono Hamas huko Gaza na Hezbollah nchini Lebanon.

Kadhalika, kundi la waasi la Houthi nchini Yemen lilitangaza iwapo Marekani itaingilia moja kwa moja mzozo kati ya Israel na kundi la waasi la Hamas, watapigana pamoja na kundi la Hamas. Wanamgambo hawa wa Houthi pia wanaungwa mkono na Iran.

Akizungumza katika bunge la Israel, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitoa onyo kwa Hamas na Hezbollah. Makundi haya yote mawili yenye silaha yanachukuliwa kuwa wawakilishi wa Iran.

Ashwini Mohapatra anasema, "Marekani na Israel hazitaki ushawishi wa Iran uongezeke katika eneo la Asia Magharibi. Ndio maana inataka kuiweka pembeni Iran."

Wataalam wanaamini makundi yenye silaha kama Hezbollah yanaleta tishio kubwa kwa Israeli kuliko Iran.

''Katika miaka mitano iliyopita, Iran imekuwa ikitekeleza azma yake kupitia makundi yenye silaha ikiwemo Hezbollah bila ya kuendesha vita vya moja kwa moja,'' anasema Mohapatra.

Vita vya Hamas-Israel ni ushindi kwa Iran?

O

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Baadhi ya wachambuzi wanaona huu ni ushindi kwa Iran baada ya kundi la wanamgambo wa Hamas kuishambulia Israel.

Kwa shambulio hili, suala la Palestina kwa mara nyingine tena limekuwa mada katika uga wa kimataifa. Na sauti za kutaka Palestina itambuliwe kama taifa zinazidi kusikika.

"Iran, ambayo sasa inaunga mkono kundi la wapiganaji la Hamas, hapo awali iliunga mkono Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina (PLO). Madai yaliyotolewa na Jumuiya ya Ukombozi wa Palestina sasa yanaibuliwa na kundi la waasi la Hamas. Haya yote yameipa nguvu Iran," anasema.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?