Kutoka kuwa mfanyakazi wa hoteli, mpaka kumiliki hoteli ya thamani ya mabilioni


Souadou Niang

CHANZO CHA PICHA, SOUADOU NIANG

Akiwa na miaka 18, Souadou Niang aliiacha familia yake na kwenda nchini Marekani. Ugunduzi huu wa Amerika ulimfungulia fursa za kitaalam ambazo zilimuwezesha kufanikiwa 

\"\" Kama hujui wewe ni nani, simama mbele ya kioo kisha jiulize swali kwasababu wewe pekee unaweza kulijibu.\"\"

Hii ni moja ya sentensi ambazo amezichukua kutoka kwa mama yake.

Mama yake Souadou aliweka mtihani huu wa kioo kwa binti yake ili kumsaidia kujichunguza mara kwa mara.

Mama kama mfano mzuri wa kuigwa

Mama yake Souadou

CHANZO CHA PICHA, SOUADOU HAS

Akiwa bila baba akiwa na miaka 3, na mtoto wa kumi na mbili katika familia ya watu 13, Souadou ni pacha.

Anasema alirithi kutoka kwa mama yake ladha yake ya "uzuri na uboreshaji. Na nguvu yake ya tabia:" alikuwa mkali sana lakini na upendo mwingi.

"Mama yangu, aliolewa, alikuwa na miaka kumi na nne na baba yangu alikuwa na miaka ishirini. Walikuwa mmoja wa weusi wa kwanza kuishi katika bandari katika jengo la wafanyakazi wa reli. Kulikuwa na wake wa raia wa Ufaransa waliomfundisha kushona, mapishi ya vyakula vya magharibi.

Yeye hakuwahi kusoma au kitu chochote lakini alijua jinsi ya kuzoea mazingira. Alikwenda kwenye sinema, alikuwa tayari kujifunza. "

Lakini kifo cha baba yake akiwa kazini ghafla kinaondoa picha hiyo nzuri. 

Mama ya Souadou anapigania kulisha na kuelimisha familia, akisaidiwa na wazee wa watoto.

Alifanya biashara ndogondogo ambayo inamruhusu kutosheleza mahitaji yake lakini huwapatia kila mmoja wa wanawe wanaofanya kazi sehemu ya bajeti ya familia: "Nakumbuka, ndugu zangu, walifanya kazi kwa bidii .\"\"

Baada ya shahada yake, anamtuma Souadou kujiunga na mmoja wa kaka zake ambaye amekaa Marekani ili aweze kuendelea na masomo yake huko.

Shabiki wa tamthilia za mahakama, Souadou alijiona kama wakili.

Lakini kukaa huko Ritz Carlton katika harakati zake za kufanya kazi ya wanafunzi kutabadilisha maisha yake.

Aliinuka kwa safu, akienda kutoka kwa mfanyakazi wa kawaida kuwa meneja, kwa sababu aliona watu wa mataifa tofauti wakisonga mbele katika taaluma yao.

"Maono yangu nilikuwa nataka kuwa katika usimamizi. Kwa sababua kulikuwa na Wamexico, Waghana ambao walikuwa katika usimamizi (...) Nilisema kwamba kama Msenegal nilikuwa na nafasi yangu."

Ilikuwa wakati huu ndipo wazo la kuunda hoteli ya kifahari nchini Senegal likaanza kuota akilini mwake. Anasema alitaka kutoa uzoefu huu wa kifahari kwa Wasenegal na Waafrika kwa ujumla: "ilikuwa katika miaka kumi ambayo nilikuwa huko ndipo nilianza kuwa na ndoto hii."

Baada ya mazungumzo marefu ya simu na mama yake, Souadou alimtakia usiku mwema. Anaahidi kumpigia simu siku inayofuata. Ni saa tatu huko huko Dakar. Haya yatakuwa mazungumzo ya mwisho kati yake na mama yake.

Souadou anafahamishwa juu ya kifo chake siku inayofuata. Kisha anaamua kurudi na mtoto wake kuhudhuria mazishi.

Tuko 2002. Anawasili Senegal baada ya mazishi na anaamua kwenda kutafakari kwenye kaburi la mama yake. lilikuwa jambo lililompa kiwewe ambao hakurudia tena.

Anasema yeye hutembelewa na mama yake ambaye humtazama kila wakati kwa kumuongoza.

Siku zake za kuomboleza zimemchosha, lazima aende nyumbani lakini anaamua kukaa.

Anapata kazi katika kampuni ya madini. Na ishara njema ya hatima yake inamfanya aamini hata zaidi katika mradi wake: "mara moja nilikuwa nimehifadhi vyumba vingi katika hoteli na kwa bahati mbaya Mfalme wa Morocco anaamua kuja Dakar na tukawatoa wawekezaji wangu wote nje ya hoteli na sikuwa na mahali pa kuwaweka. Nilisema hiyo haiwezekani. "

Ufadhili wa kifedha

Akiwa na mpango wake wa kibiashara , alikwenda kwenye benki kupata ufadhili

CHANZO CHA PICHA, SOUADOU NIANG

Mikutano imefanywa, haina matunda. Kupata karibu faranga za CFA bilioni wakati huna dhamana thabiti ya kuwekeza katika sekta ya hoteli sio rahisi.

Anakabiliwa na vikwazo vya ujasiriamali

Hii haizuiii kuanza, hata hivyo. Alilipa ada ya kukodisha kwa ambayo baadaye ingekuwa hoteli ya kifahari ya Palms boutique na akaanza kufanya kazi.

Mahojiano ya kumi na moja na benki yameandaliwa.

Wakati huu, mkurugenzi wa taasisi hii yuko Dakar na anashiriki katika mkutano huo.

Wakati Souadou anasimulia maelezo ya mkutano huu, kauli yake ilikuwa ya kushawishi. Tunaweza kugundua kwa urahisi kuwa alikuwa akitumia nafasi hiyo kwa usahihi: "ananiambia unapozungumza naona ch naona kwamba unakwenda kufaulu katika mradi huu."

Ripoti ya mkopo imewekwa. Souadou mwishowe anapata ufadhili wake.

Mara tu baada ya hatua hii kufikiwa, bado kuna changamoto nyingine za kushinda, hasa ile ya ubora wa huduma.

Hoteli za kifahari zinalenga wateja wanaohitaji, wa ulimwengu wote, waliozoea ubora wa huduma inayotolewa, kutoka mapokezi hadi malazi.

In Senegal, tourism is a key sector in the government\"s growth strategy. According to the National Agency for Statistics and Demography, it generated revenue of 275.7 billion in 2018 and employs tens of thousands of people.

Nchini Senegal, utalii ni sekta muhimu katika mkakati wa ukuaji wa serikali. Kulingana na Wakala wa Kitaifa wa Takwimu , ilizalisha mapato ya bilioni 275.7 mnamo 2018 na inaajiri makumi ya maelfu ya watu.

Yeye hufanya kazi katika hoteli kubwa huko Dakar wakati anasikia juu ya mradi wa Souadou. Anafanikiwa kupata nambari yake na kumpigia ili ampe huduma.

Palms wakati huo ilikuwa eneo la ujenzi tu

Hatahivyo, wanaendelea kuwasiliana.

Hadi siku alipopokea simu kutoka kwa Souadou ambaye anamtake aende kuona maendeleo ya kazi.

Yeye ndiye mfanyakazi wa kwanza wa hoteli hiyo, ambayo sasa ndiye msimamizi.

Licha ya uzoefu wake, Souadou anasema alimlipa kukaa wiki moja katika kasri la Morocco na wenzake wengine ili waweze kupata uzoefu wa wateja katika hoteli za kiwango cha juu: "Tuliwapa huduma nzuri tuliwaonesha namna ya kumpokea mteja. Wenyewe walikuwa watej. Ilibidi niwapeleke huko, ili waweze kuelewa ninachotaka ili niweze kuliachia jukumu.

Janga la corona

Hoteli hiyo ilifungua milango yake mnamo 2017 na inavutia wateja wa Anglo-Saxon.

Biashara inaenda vizuri, amefanikiwa kuwalipa wafanyikazi wake. Hadi janga la corona linatokea. Hoteli hiyo bado imefungwa kwa miezi kumi na moja.

"Ilikuwa ngumu. Bado ni ngumu kwa sababu tulifunga Machi 10, 2020, serikali ilitutaka tufunge lakini tayari tulikuwa tumeanza kuhisi shida ya Covid. Kwa sababu wachimbaji walikuja kutoka Australia na walikuwa wakipitia Asia kufika. Na mimi , tangu Oktoba 2019 nilikuwa nimehisi kushuka sana. "

Licha ya kufunguliwa tena, sehemu kubwa ya wateja wake bado haijarudi kwa sababu ya vizuizi vya kusafiri katika muktadha huu wa janga hilo.

Alipata msaada kutoka Senegal "mkopo uliocheleweshwa zaidi ya miaka miwili kulipa miezi mitatu ya mshahara wa kwanza wa kufunga."

Anatarajia kufaidika na mfuko wa msaada wa Force Covid ulioanzishwa na serikali: "tumejaza fomu zote, tunasubiri."

Kulingana na ripoti ya pamoja ya UNCTAD na UNWTO iliyochapishwa mnamo Juni 30, 2021, kuanguka kwa utalii wa kimataifa kwa sababu ya janga hilo kunaweza kugharimu uchumi wa dunia kisi cha dola trilioni 4 mnamo 2020 na 2021.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Umoja wa Ulaya hatimaye wakubaliana kuufufua uchumi wao

Urusi kuisadia Uganda kujenga uwezo wake wa nyuklia, ni mataifa gani ya Afrika yanatumia nishati ya nyuklia na kwanini?