Uchaguzi Tanzania 2020: Je, namna gani wapiga kura wanaweza kuepuka migogoro wakati wa kampeni?
Matukio ya vurugu za kisiasa miongoni mwa wapiga kura wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa urais,ubunge na udiwani unaoendelea nchini Tanzania yameathiri mahusiano moja kwa moja kutokana na itikadi tofauti za vyama vya siasa licha ya Katiba ya nchi hiyo kusisitiza uhuru wa kila mwananchi katika kuchagua itikadi hizo pamwe na kudumisha misingi ya demokrasia na siasa za vyama vya vingi. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na matamko ya vitisho dhidi ya wafuasi na wanasiasa wa pande mbili tofauti, kujinyonga, kupigana kwa kutumia mapanga na silaha zingine za jadi hali ambayo inachochea uvunjaji wa sheria pamoja na kuibua taharuki miongoni mwa familia, ndugu, marafiki na taifa kwa ujumla. Duru za kisiasa zimetafsiri hali hiyo ni kiwango duni cha uvumilivu wa kisiasa miongoni mwa wapigakura, na kusababisha baadhi ya wapiga kura kuchukua uamuzi wa kukatisha uhai wao kwa sababu ya kutokukubaliana na wengine ndani ya familia, pamoja na viongozi kushindwa kuwa na lugha za ushawishi wafuasi ...