Kifo cha George Floyd: Wakili akiita 'mauaji yaliyopangwa'
Wakili wa familia ya George Floyd, ambaye kifo chake kiliibua maandamano ya hasira kote nchini Marekani , amemshutumu afisa wa polisi kwa "kupanga mauaji". Polisi wa Minneapolis Derek Chauvin ameshitakiwa kwa mauaji , lakini wakili Benjamin Crump amekiambia kituo cha habari cha CBS news kuwa yalikuwa ni mauaji ya kiwango cha kwanza. "Tunadhani kwamba alikua na nia … takriban dakika tisa aliendelea kushindilia goti lake kwenye shingo ya mwanaume ambaye alikua anamuomba amsamehe na kumwambia kuwa hawezi kupumua," alisema matukio ya uporaji yameripotiwa katika jimbo la Philadelphia. Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya polisi na kuiba katika duka moja . Ripoti ya Uchunguzi ya West Philadelphia, imesema kuwa magari ya polisi pia yalichomwa moto. Miji kadhaa ya Marekani imeweka amri ya kutotoka nje. Rais Donald Trump alituma ujumbe wake wa twitter uliosema: Sheria na amri v...