Machapisho

Kwanini Somaliland ina matumaini na ujio wa Trump?

Picha
CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo kuhusu taarifa Author, Watu wengi huko Somaliland wanaamini kwamba Marekani, chini ya rais ajaye Donald Trump, itakuwa nchi ya kwanza duniani kuitambua jamhuri hiyo iliyojitangazia uhuru wake. Eneo hilo lilijitangazia uhuru miaka 33 iliyopita baada ya Somalia kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. "Donald ni mwokozi wetu. Ni mtu mwenye hekima. Mungu ibariki Marekani," anasema mwanafunzi wa chuo kikuu Aisha Ismail. Anazungumza nami kutoka Hargeisa, mji mkuu wa Somaliland - jiji lililo umbali wa kilomita 850 (maili 530) kaskazini mwa Mogadishu, Somalia. Kwa wale walio Mogadishu, Somaliland ni sehemu ya Somalia. "Nina shaka kwamba Donald Trump anaijua Somaliland ni nini, au iko wapi," anasema Abdi Mohamud, mchambuzi huko Mogadishu. Pia unaweza kusoma Wakuu wa jeshi la Ethiopia-Somaliland wakutana huku kukiwa na mvutano wa kikanda 9 Januari 2024 Makubaliano ya Ethiopia na Somaliland yatikisa diplomasia katika Pembe ya Afrika 9 Janu...

Ukigundua una dalili hizi 10 nenda ukapimwe maradhi ya Kisukari

Picha
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Afroza Akhtar hakuelewa kwamba alikuwa na kisukari kwa muda mrefu. Hakujua kwamba sababu za kujihisi kiu, uchovu na mwili kuishiwa nguvu huenda ni baadhi ya dalili za maradhi hayo. ''Nilikwenda kwa daktari na kumueleza baada ya kujisikia vibaya kwa muda mrefu.Alinifanyia vipimo vya kisukari na magonjwa mengine. Ni pale ndipo niligundulika kuwa nina ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu '' Tangu hapo alianza matibabu katika hospitali maalum ya ugonjwa wa kisukari. Si yeye pekee, kwa mujibu wa wataalamu wa kisukari, zaidi ya asilimia 50 ya watu wenye maradhi ya kisukari hawafahamu kuwa wana ugonjwa huo MATANGAZO Ugonjwa huo uligunduliwa wakati wa alipokuwa akipimwa maradhi mengine. Unaweza pia kusoma Ni rahisi kuepuka ugonjwa wa kisukari? 14 Novemba 2021 Ugonjwa wa kisukari unaweza kutibika na kuzuiwa kirahisi - Daktari anaeleza 7 Machi 2024 Wataalamu wanasema kutokana na hali hiyo ndiyo maana ni muhimu sana kutoa hamasa kwa jamii kuhusu ugonjw...

Israel ina mpango wa kutaka kuitwaa Gaza kaskazini

Picha
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Magazeti kadhaa ya Kiarabu, Uingereza na Marekani yaliangazia matokeo ya kurejea kwa Donald Trump katika kiti cha urais nchini Marekani kwa eneo la Mashariki ya Kati. Katika muktadha huu, Makala haya yanaangazia kuhusu hofu ya Israel kunyakua ardhi ya Palestina, na kwa upande mwingine kuhusu safu ya viongozi wapya wa Trump. Pia utafahamu kuhusu mwelekeo wa uhusiano kati ya Trump na Iran katika siku za usoni. Tunaanza na gazeti la Uingereza The Guardian na makala iliyoandikwa na Ben Reeve, ambapo aliangazia matamshi, harakati za kijeshi, na hatua za kisiasa ambazo zinaonyesha kuwa Israeli inapambana kunyakua Ukanda wa kaskazini mwa Gaza. MATANGAZO Mwandishi wa gazeti la Uingereza alirejelea matamshi ya Itzik Cohen, afisa mkuu wa jeshi la Israel, aliyoyaona kama "ukiri" kwamba Israel inatekeleza "maangamizi kwa jamii hiyo ya kaskazini mwa Gaza, na kuuhadaa ulimwengu kuhusu malengo yake halisi katika eneo ililodhibiti. Makala hiyo ilieleza kwa...