Machapisho

Maandamano Kenya: 'Msiwaue, wapigeni risasi mguuni' Ruto awaambia polisi

Picha
BBC News,  Swahili CHANZO CHA PICHA, Rais wa Kenya William Ruto ameapa kutumia ''mbinu zozote zinazohitajika'' kuhakikisha amani na utulivu inadumishwa nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa makazi ya polisi jijini Nairobi Rais Ruto aliyeonekana kuwa na hasira alisema yuko tayari kufanya lolote kukomesha wimbi la maandamano ya machafuko la hivi majuzi ambalo limesababisha vifo vya zaidi ya watu 40. "Inatosha, hatuwezi kuruhusu hili liendelee, tutatumia njia zozote kuleta utulivu nchini," alisema. Kenya imeshuhudia wimbi la maandamano dhidi ya serikali, ambayo yalianza Juni 2024 kupinga nyongeza ya kodi. Maandamano hayo, hasa yakiongozwa na vijana, wanaofahamika 'Gen-z' hata hivyo yamebadilika na kujumuisha wito wa kumtaka Rais Ruto ajiuzulu, kukomesha ukatili wa polisi na utawala mbaya. Katika hotuba yake ya kwanza kwa umma kuhusu suala hilo, tangu duru ya hivi punde zaidi ya maandamano mapema wiki hii alisema, ''Ni viongozi wanaowa...

Rwanda bila misaada: Je, inaweza kujitegemea?

Picha
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Hivi karibuni nchi za Ulaya, Marekani na Canada zimekuwa zikitangaza hatua ya kukata misaada dhidi ya Rwanda, kufuatia kile kinachoelezwa na nchi hizo za Magharibi kwamba inaunga mkono kundi la M23 liloteka maeneo ya mashariki mwa DRC, ikiwemo miji ya Goma na Bukavu. Nchi hizo zinaituhumu Rwanda kuchochea ghasia katika eneo la Mashariki mwa DRC kwa kuwaunga mkono waasi wa kitutsi wa Congo wa kundi la M23, tuhuma zinazokanushwa vikali na Rwanda. Lakini je, Rwanda inaweza kujitegemea bila misaada? Kujibu swali hili ni vyema kuelewa ni kwa namna gani Rwanda inategemea misaada kutoka mataifa ya kigeni kwa ajili ya kuendesha uchumi wake. Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia, Rwanda ilikadiriwa kutegemea kwa kiasi kikubwa misaada ya kigeni mnamo 2024, huku makadirio yakionyesha kuwa misaada na mikopo kutoka nje inaweza kuchangia na karibu 27% ya jumla ya bajeti ya taifa hilo. Inakadiriwa kuwa Rwanda inapokea zaidi ya dola bilioni 1 ya msaada wa kigeni Pia una...

Kwanini Somaliland ina matumaini na ujio wa Trump?

Picha
CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo kuhusu taarifa Author, Watu wengi huko Somaliland wanaamini kwamba Marekani, chini ya rais ajaye Donald Trump, itakuwa nchi ya kwanza duniani kuitambua jamhuri hiyo iliyojitangazia uhuru wake. Eneo hilo lilijitangazia uhuru miaka 33 iliyopita baada ya Somalia kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. "Donald ni mwokozi wetu. Ni mtu mwenye hekima. Mungu ibariki Marekani," anasema mwanafunzi wa chuo kikuu Aisha Ismail. Anazungumza nami kutoka Hargeisa, mji mkuu wa Somaliland - jiji lililo umbali wa kilomita 850 (maili 530) kaskazini mwa Mogadishu, Somalia. Kwa wale walio Mogadishu, Somaliland ni sehemu ya Somalia. "Nina shaka kwamba Donald Trump anaijua Somaliland ni nini, au iko wapi," anasema Abdi Mohamud, mchambuzi huko Mogadishu. Pia unaweza kusoma Wakuu wa jeshi la Ethiopia-Somaliland wakutana huku kukiwa na mvutano wa kikanda 9 Januari 2024 Makubaliano ya Ethiopia na Somaliland yatikisa diplomasia katika Pembe ya Afrika 9 Janu...