Dini ya Kiislamu kuipiku ile ya Kikristo kwa ukubwa 2070
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Waislamu wakifanya ibada. Utafiti unasema kuwa dini ya Uislamu inatarajiwa kuipiku ile ya Wakristo ifikiapo 2070 Uislamu ni dini ya pili kwa ukubwa baada ya Ukristo kwa sasa lakini inakua kwa haraka sana. Hata hivyo hilo huenda likabadilika iwapo mwenendo wa watu wanaojiunga na dini hiyo utaendelea, kulingana na utafiti uliochapishwa na kituo cha utafiti cha Marekani Pew Research Center. Kulingana na utafiti huo Uislamu unakuwa kwa haraka ikilinganishwa na dini nyengine yoyote ile duniani. Itaipiku dini ya Kikristo ifikiapo 2070 kulingana na makadirio yake na hivyobasi kuwa dini yenye ufuasi mkubwa duniani. MATANGAZO Umoja wa Wakristo na Waislamu Kibera Mkahawa wakataa kuwahudumia wanawake Waislamu Ufaransa Msikiti mkubwa Afrika wajengwa Algeria Mwaka 2010 taifa la Indonesia ndilo taifa lililokuwa na idadi kubwa ya Waislamu duniani lakini sasa India huenda ikawa na wafuasi wengi zaidi duniani ifikiapo 2050. Hatahivyo taifa hilo litakuwa ...