Kombe la dunia : Afrika haina viwanja vya mechi za kombe la dunia
Saa 2 zilizopita CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Kupigwa marufuku kwa viwanja kadhaa vya soka barani Afrika huenda kutaathiri mechi za ufunguzi za kufuzu kwa Kombe la Dunia la Afrika mnamo Juni. Jumla ya mataifa 10 kati ya 40 yanayoshiriki katika kampeni ya kufuzu yanakabiliwa na tishio la kushiriki mechi nje ya mipaka yao . Hii ni baada ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) kutuma barua kwa mashirikisho wanachama wiki hii iliyokuwa na orodha ya viwanja vilivyoidhinishwa kwa raundi mbili za kwanza za mechi za makundi. Nchi zilizoathiriwa ni pamoja na Senegal, ambao walishiriki kwenye Kombe la Dunia lililopita huko Urusi mnamo 2018, na Mali, ambao walikuwa miongoni mwa timu zilizoshinda nafasi ya kwanza. MATANGAZO Tetesi za soka Ulaya Jumatano 05.05.2021 Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Liberia, Malawi, Mali, Namibia, Niger na Sierra Leone zote hazijaidhinishiwa viwanja vyao vya nyumbani wakati Caf inapokabiliana na miundombinu mibovu kote barani. Sasa timu hizo zina muda mf...