Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2017

Mwanamke aliyetiwa pingu atoroka na gari la polisi

Maafisa wa polisi wa Texas walipomuingiza mwanamke huyu ndani ya gari lao la kushika doria, walitarajia angetulia na hawakumjali hadi waliposhtukia amevurumisha gari lao na kuondoka nalo. Alikimbizwa kwa zaidi ya dakika 23 akiendesha gari hilo kwa kasi ya zaidi ya maili 100 kwa saa. Mwishowe alishinda kudhibiti gari.

Asernal manager, Arsene Wenger aongeza mkataba mpya

Picha
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekubali kuchukua mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo, hatua itakayoendeleza muda ambao amekaa katika klabu hiyo. Mfaransa huyo amekuwa meneja wa Arsenal kwa miaka 21 sasa. Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke walikutana Jumatatu kuamua hatima ya meneja huyo, na kisha uamuzi wao ukawasilishwa kwa mkutano wa bodi Jumanne. Arsenal wanapanga kutangaza rasmi uamuzi huo Jumatano. Gunners walimaliza Ligi ya Premia wakwia nafasi ya tano, mara yao ya kwanza kumaliza chini ya nafasi ya nne tangu Wenger alipojiunga nao mwaka 1996. Walimaliza alama 18 nyuma ya mabingwa Chelsea, lakini walifanikiwa kuwachapa Blues katika fainali ya Kombe la FA uwanjani Wembley Jumamosi. Mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu. Wenger: Sitasoma kitabu cha Mourinho Mourinho: Nafurahi mashabiki wa Arsenal walifurahi Wenger aliongoza Gunners kushinda mataji matatu ya Ligi ya Premia na pia vikombe vinne vya FA misimu yake tisa ya kwanza kweny

Yanga wamlilia Manji

Picha
WANACHAMA wa Yanga wamemuangukia mwenyekiti wao aliyejiuzulu Yusuf Manji baada ya kukataa ombi la kuachia ngazi la kiongozi huyo. Wanachama wa klabu hiyo kutoka matawi 65 ya mkoa wa Dar es Salaam walikutana jana na kumtaka makamu mwenyekiti wao, Clement Sanga kuhitisha haraka kmkutano wa dharura. Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambapo kwa pamoja waliazimia kukataa ombi la kujiuzulu kwa Manji. “Wanachama hawataki Manji akae pembeni, wanataka mkutano wa dharura uitishwe siku 14 toka leo kwa mujibu wa katiba, kamati ya utendaji inakaa leo ( Jana) mchana itapitia maombi ya wanachama na kutoa maamuzi.” alisema Mkwasa. Naye Makamu Mwenyekiti wa matawi Bakili Makele alisema kuwa baada ya kutafakari barua ya Manji, ambayo inaeleza moja ya sababu ya kujiuzulu ni kutokana na afya yake, lakini wao wanasema bado wanamuhitaji. Naye Mwenyekiti wa Keko Ukombozi Joseph Kalindwa akizungumzia hilo alisema “ Manji alitukuta kipindi kigumu mno tukiwa tumegubikwa na mgog

Trump anakutana na Papa Francis

Picha
Rais Donald Trump anatarajiwa kuzungumza na Papa Francis na viongozi nchini Italia mjini Roma katika awamu ya tatu ya ziara yake baada ya kuingia madarakani. Trump na kiongozi huyo wa kidini tayari wame tofautiana kiasi kuhusu masuala yakiwemo uhamiaji na mabadiliko ya tabia nchi. Kiongozi huyo wa Marekani anakutana pia na rais wa Italia na waziri mkuu, kabla ya kuelekea Brussels kwa mkutano wa jumuiya ya kujihami NATO. Awali aliapa kufanya kila awezalo kuisaidia Israel na Palestina kuidhinisha amani alipokamilisha ziara yake mashariki ya kati. Pope Francis.Haki miliki ya pichaAFP Image caption Papa Francis ameshutumu hatua ya rais Trump kujenga ukuta katika mpaka baina ya Mexico na Marekani Papa Francis na Rais Trump ni viongozi wawili walio na tofauti kubwa. Upande mmoja Papa ameelekeza maisha yake kutetea maskini na wasiojiweza na upande mwingine mfanyabiashara, Rais Trump amelenga kutajirika na amejihusisha na mabilionea katika baraza lake la mawaziri. Na licha ya kwamba h