Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2023

Je, Iran ina nguvu ya kuingia vitani moja kwa moja na Israel?

Picha
Je, Iran ina nguvu ya kuingia vitani moja kwa moja na Israel? CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Maelezo ya picha, Suali linaloulizwa na wengi, ni ikiwa Iran inao uwezo wa kuingia vitani na Israel 27 Oktoba 2023 Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameionya hadharani Israel - ni lazima isitishe mashambulizi yake huko Gaza la sivyo italazimika kuchukua hatua. Ndani ya masaa machache baadaye, Iran ilibadilisha msimamo katika Umoja wa Mataifa - ikasema haitaingilia mzozo kati ya Israel na Hamas ila ikiwa tu maslahi ya Iran na raia wake yataathirika. Hata hivyo, katika mzozo huu wa pande mbili, Iran tangu awali imeeleza wazi uungaji mkono kwa kundi la wapiganaji wa Hamas na Wapalestina. Pia inaionya Israel huenda ikakabiliwa na matokeo mabaya. Naibu kamanda wa jeshi la Iran, aliitishia Israel kwa shambulio la kombora katika mji wa Haifa nchini Israel. Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amesema iwapo mashambulio ya Israel dhidi ya Gaza yataendelea hakuna mtu atakayeweza kuwazuia Waislamu, k