Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2022

Ushindi wa William Ruto nchini Kenya unafundisha nini Tanzania?

Picha
​ Baada ya kuwatumikia Wakenya kwa miaka kumi akiwa Naibu wa Rais, sasa Bwana William Ruto ni rais mteule ambaye Wakenya wamempa kazi kubwa zaidi ya kuwa rais kwa miaka mitano ijayo; iwapo mambo yataendelea kubaki kama yalivyo sasa. Ruto wa muungano wa Kenya Kwanza amemshinda mwanasiasa mkongwe bwana Raila Odinga, wa Azimio la Umoja kwa kupata asilimia 50.49 dhidi ya asilimia 48.85 za kura halali. Ushindi huo umemfanya Ruto kuwa mrithi wa kiti cha urais kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta akingojea kuapishwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wake wa Twitter amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu. Pia, akaahidi kuwa Tanzania itaendeleza udugu na ushirikiano wa kihistoria wa mataifa hayo. Changamoto za ujirani  Kenya ni ileile, jirani wa Tanzania. Kwa sasa kinachokwenda kubadilika ni kiongozi tu atakayeliongoza taifa hilo la wakazi zaidi milioni 54 kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia za mwaka 2021. Wakati haya