Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2022

Tunachokifahamu kufikia sasa kuhusu shambulio la Alshabab dhidi ya wanajeshi wa Burundi.

Picha
​ Kundi la Kigaidi la al-Shabab limesema kuwa wao ndio wahusika kwenye mauaji makubwa katika shambulizi la katika kambi ya walinda amani wa Umoja wa Afrika nchini Somalia, hata hivyo pande zote mbili zimekuwa zikitoa taarifa zinazokidhana juu ya idadi za vifo. Kundi hilo ambalo ni washirika wa al-Qaeda wamesema wamewaua wanajeshi wapatao 170 wa AU, wengi wao wakiwa wametokea nchini Burundi pia kuwaweka mateka wengine bila kutaja idadi yao.  Hata hivyo jeshi la Burundi limesema kuwa wanajeshi wake 10 ndio waliopoteza maisha na wengine watano waliopotea. Bado mpaka sasa hakuna taarifa za uhakika kuhusu shambulizi hili. MATANGAZO Kitu gani kilitokea kwenye shambulio hilo? Mashambulizi hayo katika eneo la Shabelle ya Kati nchini humo yalishuhudia wapiganaji waliokuwa na silaha nzito wakivamia kambi ya al-Baraf kilomita 160 kaskazini-mashariki mwa mji mkuu, Mogadishu, ambako vikosi vya Burundi, vinavyohudumu chini ya AU, viliweka kambi. Wananchi wa eneo hilo wanadai kusikia milio ya silaha

Vikwazo vya magharibi vyawakimbiza matajiri wa Urusi kwenda Dubai