Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2022

Habari za moja kwa moja

Picha
​ Mtoto auawa Nigeria katika jaribio la 'kuzuia risasi' kwa kuvaa hirizi AFP Copyright: AFP Mvulana miaka 12 kutoka Nigeria ameuawa na kaka yake alipokuwa akijaribu hirizi mpya ya "kuzuia risasi", polisi wanasema.  Wawili hao waliamini kuwa "wamejiimarisha kwa hirizi ya ulinzi", kwa mujibu wa polisi katika jimbo la Kwara, Abubakar Abubakar kisha akampiga risasi mdogo wake Yusuf, 12, kwa kutumia bunduki ya baba yao, maafisa wanasema.  Mvulana huyo alipigwa risasi na bunduki ya kizamani inayojulikana kama dane gun, polisi wanasema. Polisi sasa wanamsaka anayedaiwa kuwa muuaji. Licha ya ukosefu wa ushahidi, hirizi hutumiwa na baadhi ya watu nchini Nigeria ambao wanataka ulinzi dhidi ya matukio mabaya.  Kumekuwa na ripoti kadhaa za watu kuuawa baada ya kupima hirizi na dawa za kishirikina za kuzuia risasi. Haijabainika kwa nini ndugu hao wawili walienda kupata ulinzi. Yusuf Abubakar inasemekana alifariki dunia papo hapo baada ya kupigwa risasi huku kak yake mkub

Ushindi wa William Ruto nchini Kenya unafundisha nini Tanzania?

Picha
​ Baada ya kuwatumikia Wakenya kwa miaka kumi akiwa Naibu wa Rais, sasa Bwana William Ruto ni rais mteule ambaye Wakenya wamempa kazi kubwa zaidi ya kuwa rais kwa miaka mitano ijayo; iwapo mambo yataendelea kubaki kama yalivyo sasa. Ruto wa muungano wa Kenya Kwanza amemshinda mwanasiasa mkongwe bwana Raila Odinga, wa Azimio la Umoja kwa kupata asilimia 50.49 dhidi ya asilimia 48.85 za kura halali. Ushindi huo umemfanya Ruto kuwa mrithi wa kiti cha urais kutoka kwa Rais Uhuru Kenyatta akingojea kuapishwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kupitia ukurasa wake wa Twitter amewapongeza wananchi wa Kenya kwa kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu. Pia, akaahidi kuwa Tanzania itaendeleza udugu na ushirikiano wa kihistoria wa mataifa hayo. Changamoto za ujirani  Kenya ni ileile, jirani wa Tanzania. Kwa sasa kinachokwenda kubadilika ni kiongozi tu atakayeliongoza taifa hilo la wakazi zaidi milioni 54 kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia za mwaka 2021. Wakati haya