Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2021

Marekani na Ulaya zaonya wanajeshi wa Eritrea kuingia Tigray

Picha
Marekani na Umoja wa Ulaya zimeelezea wasiwasi wao kuhusu kupelekwa hivi karibuni kwa majeshi ya Eritrea kwenye jimbo la Tigray nchini Ethiopia, ambako pameshuhudiwa vita vilivyodumu kwa miezi tisa. Vikosi kutoka Tigray vilidhibiti tena eneo kubwa la jimbo hilo mwezi Juni, ikiwa ni pigo kubwa kwa serikali ya Ethiopia. Lakini kupelekwa tena kwa vikosi vya Eritrea, miezi kadhaa baada ya Ethiopia kusema majeshi ya kigeni yalikuwa yakiondoka, kunazusha hofu ya kuongezeka mapigano zaidi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema nchi yake ina wasiwasi kwamba idadi kubwa ya majeshi ya ulinzi ya Eritrea yameingia tena Ethiopia, baada ya kuondoka mwezi Juni. Blinken ameyatoa matamshi hayo wakati ambapo wizara ya fedha ya Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya mkuu wa jeshi la Eritrea anayetuhumiwa kwa kukiuka haki za binaadamu wakati wa vita vya Tigray. Eritrea imesema madai hayo hayana msingi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken Wakati huo huo, Agosti 20, mabaloz