Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2025

Rwanda bila misaada: Je, inaweza kujitegemea?

Picha
CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES Hivi karibuni nchi za Ulaya, Marekani na Canada zimekuwa zikitangaza hatua ya kukata misaada dhidi ya Rwanda, kufuatia kile kinachoelezwa na nchi hizo za Magharibi kwamba inaunga mkono kundi la M23 liloteka maeneo ya mashariki mwa DRC, ikiwemo miji ya Goma na Bukavu. Nchi hizo zinaituhumu Rwanda kuchochea ghasia katika eneo la Mashariki mwa DRC kwa kuwaunga mkono waasi wa kitutsi wa Congo wa kundi la M23, tuhuma zinazokanushwa vikali na Rwanda. Lakini je, Rwanda inaweza kujitegemea bila misaada? Kujibu swali hili ni vyema kuelewa ni kwa namna gani Rwanda inategemea misaada kutoka mataifa ya kigeni kwa ajili ya kuendesha uchumi wake. Kulingana na takwimu za Benki ya Dunia, Rwanda ilikadiriwa kutegemea kwa kiasi kikubwa misaada ya kigeni mnamo 2024, huku makadirio yakionyesha kuwa misaada na mikopo kutoka nje inaweza kuchangia na karibu 27% ya jumla ya bajeti ya taifa hilo. Inakadiriwa kuwa Rwanda inapokea zaidi ya dola bilioni 1 ya msaada wa kigeni Pia una...