Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2021

Mshirika wa Trump Erik Prince alikiuka vikwazo vya kuingiza silaha Libya

Picha
Ripoti ya siri ya Umoja wa Mataifa inadai kwamba Prince alimsaidia mbabe wa kivita wa Libya Khalifa Haftar kwa kumpatia silaha na mamluki wa kimataifa. Mkandarasi binafsi wa masuala ya usalama na mshirika la rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, Erik Prince, anatajwa kukiuka marufuku ya kuingiza silaha nchini Libya ya Umoja wa Mataifa, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, ambayo pia nakala yake imeonekana na vyombo vya habari vya Marekani. Kulingana na ripoti hiyo ya siri ya Baraza la Usalama, iliyoonekana na magazeti ya New York Times na Washington Post, Prince alipeleka kikosi cha wapiganaji mamluki na silaha kwa mbabe wa kivita Khalifa Haftar, ambae 2019 alikuwa akipigana kuiondoa madarakani serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa. Operesheni hiyo ya dola milioni 80 ilijumuisha mipango ya kuunda kikosi kitakachowafuatilia na kuwaua makamanda wa Libya wanaompinga Haftar, pamoja na wadau wengine ambao walikuwa raia wa mataifa ya Umoja wa Ulaya, limesema gazeti