Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2021

Maelfu ya wafuasi wa Navalny wakamatwa Urusi

Picha
Zaidi ya watu 2,100 wamekamatwa leo Jumapili wakati wa maandamano yaliyofanyika kwenye miji mbalimbali nchini Urusi kushinikizwa kuachiwa kwa kiongozi wa upinzani aliye kizuizini Alexei Navalny. Maandamano zaidi yanatarajiwa kwenye mji mkuu Moscow, na tayari mamlaka za mji huo zimeamuru kufungwa kwa vituo vya treni na kuweka vizuizi kwenye mitaa inayozunguka Ikulu ya Kremlin. Maelfu ya watu wamejitokeza kushiriki maandamano hayo ya  kumuunga mkono Navalny na kulaani uamuzi wa mamlaka za Urusi kumuweka korokoroni. Kulingana na kundi linalofuatilia hali ya mambo nchini Urusi, hadi mchana wa leo polisi ilikuwa imewakamata waandamanaji 2,100. Shirika la Habari la Reuters limeripoti mjini Moscow pekee watu 100 wamekamatwa. Polisi ililazimika kuufunga uwanja wa Lubyanka ulio karibu na Ikulu ya Kremlin eneo ambalo waandamanaji walipanga kukusanyika. Kutokana na hatua hiyo, waandaaji wa maandamano hayo waliwahimiza wafuasi wao kujikusanya kwenye uwanja mwingine wa wazi mjini Moscow. Polisi wam