Maandamano Kenya: 'Msiwaue, wapigeni risasi mguuni' Ruto awaambia polisi
BBC News, Swahili CHANZO CHA PICHA, Rais wa Kenya William Ruto ameapa kutumia ''mbinu zozote zinazohitajika'' kuhakikisha amani na utulivu inadumishwa nchini. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa makazi ya polisi jijini Nairobi Rais Ruto aliyeonekana kuwa na hasira alisema yuko tayari kufanya lolote kukomesha wimbi la maandamano ya machafuko la hivi majuzi ambalo limesababisha vifo vya zaidi ya watu 40. "Inatosha, hatuwezi kuruhusu hili liendelee, tutatumia njia zozote kuleta utulivu nchini," alisema. Kenya imeshuhudia wimbi la maandamano dhidi ya serikali, ambayo yalianza Juni 2024 kupinga nyongeza ya kodi. Maandamano hayo, hasa yakiongozwa na vijana, wanaofahamika 'Gen-z' hata hivyo yamebadilika na kujumuisha wito wa kumtaka Rais Ruto ajiuzulu, kukomesha ukatili wa polisi na utawala mbaya. Katika hotuba yake ya kwanza kwa umma kuhusu suala hilo, tangu duru ya hivi punde zaidi ya maandamano mapema wiki hii alisema, ''Ni viongozi wanaowa...